Friday, August 28, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili (NIT & TFS) Tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/272

27Agosti,2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya CHUO CHA USAFIRISHAJI CHA TAIFA (NIT)NA WAKALA WA MISITU TANZANIA (TFS) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe12 hadi 14 Septemba,2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i.Usaili utafanyika tarehe12 hadi 14Septemba, 2020 kamailivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kilaKada;
ii.Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa mchujo,namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya kazi.
iii.Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask);
iv.Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwaajili ya utambuzi;
Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
-Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura,

  • Kitambulisho cha kazi,
    -Kitambulisho cha Uraia au
  • Hatiyakusafiria;
    v.Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
    vi.Wasailiwa watakao wasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATA RUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
    vii.Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
    viii.Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipo pangiwakufanyia usaili;
    ix.Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikisheVyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlakahusika(kama TCU, NACTE au NECTA);
    x.Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hiliwa tambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
    xi.Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
    xii.Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
    RATIBA YA USAILI

KUONA RATIBA NA MAJINA PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili (NIT & TFS) Tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2020 appeared first on Business Solutions.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili (NIT & TFS) Tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/22102/