Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wailaya ya Bagamoyo Tarehe 21 Mei 2020
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO
Kumb.Na.HWB/A.20/76/212 08 Mei, 2020
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi
wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kufanyika tarehe 21 Mei, 2020 na hatimaye
kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili wa Mchujo, Vitendo na Mahojiano utafanyika tarehe 21 Mei, 2020, katika shule ya
Sekondari Bagamoyo iliyopo kata ya Dunda – Bagamoyo Mjini.
ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha
Mpiga kura, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato
cha IV, VI, na Astashahada kutegemeana na mahitaji ya tangazo la kazi na sifa za
Mwombaji;
v. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form iv and form vi results slips)
HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi
vii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA);
viii. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na
kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
ix. Kila Msailiwa azingatie Kuvaa Barakoa wakati wote wa Zoezi la Usaili ili kujikinga na
COVID-19 kwa kuzingatia maelekezo yalivyotolewa na Serikali.
KUONA ORODHA HIYO TAFADHALI PAKUA PDF HAPO CHINI
The post Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wailaya ya Bagamoyo Tarehe 21 Mei 2020 appeared first on Ajira Zetu.
The post Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wailaya ya Bagamoyo Tarehe 21 Mei 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.
source http://ajira-nafasizakazitz.com/16639/