Monday, March 2, 2020

Nafasi za Kazi Baylor College of Medicine Childrens Foundation, Tuma Maombi Kabla ya Tarehe 11 March 2020

Watoa Huwanyu (HBCs) (3)
Posted by: Baylor Tanzania
Posted date: 2020-Feb-21
Location: Mbeya

Nafasi za Kazi

Baylor College of Medicine Childrens Foundation – Tanzania ni shirika lisilo la Kiserikali (NGO) maalum kwa kusaidia kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu, huduma fahamishi za maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (HIV/AIDS) na matibabu kwa watoto ambao wako hatarini kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kutoka kwa mama anayeishi na Virusi Vya Ukimwi na watoto ambao tayari wamepata maambukizi kutoka kwa wazazi wao na vijana katika kanda ya Ziwa na Nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Shirika la Baylor – Tanzania linashirikiana na shirika la Baylor kimataifa linalohudumia watoto wenye maambukizi ya VVU (BIPAI) katika mtandao mzima ambao makao makuu ya chuo cha Baylor cha dawa kilichopo Houston, Texas Marekani (USA). Shirika la Baylor – Tanzania lilianzishwa na washirika wa kimarekani katika mpango wa kimataifa wa maendeleo (USAID) na linafanya kazi katika kuisaidia serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto katika kuimarisha kutoa huduma kwa watoto na vijana walioathirika na wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi katika Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania

Nafasi za Kazi: Watoa Huwanyu (HBCs) (3)
Mkoa: Mbeya

MAJUKUMU YA WATOA HUWANYU (HBCs)
• Kutafuta watoto waliozaliwa kwa wazazi wenye VVU na kujenga mahusiano mazuri kwa watu wanaoishi na maambukizi katika CTCs mbalimbali Mbeya jiji ili kuweza kupata watoto wanaohitaji upimaji wa vvu.
• Kuwasindikiza /kuwapeleka wale wanaohitaji kujua afya zao hasa watoto waliozaliwa na wazazi wanaotumia dawa ( ARVs )
• Kufuatilia na Kutoa huduma za kiafya kwa familia yenye wagonjwa wenye magonjwa sugu eg VVU.
• Kutoa elimu kwa wazazi wanaoishi na maambukizi pamoja na wasaidizi wao kuhusu matibabu ya watu wanao ishi na maambukizi .
• Kuwapa elimu kuhusu ufuasi mzuri wa dawa za kupunguza makali ya VVU (ART)
• Kufuatilia wagonjwa ambao hawakuhudhuria kliniki katika tarehe walizopangiwa na kuwaelimisha umuhimu wa kuhudhuria klinic kama walivyopangiwa .
• Kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya watoto wanaotumia dawa za vvu kila wiki katika vikao vya wiki na report za miezi mitatu.
• Kuwapa matumaini kisaikologia,kijamii,kiuchumi na kiroho kwa kuwaunganisha na wataalamu wanaoweza kuwasaidia katika shida zinazowakabili ili waweze kuishi vema ktk jamii inayowazunguka.

SIFA ZA MWOMBAJI HUWANYU HBCs
• Awe amemaliza darasa la saba ua kidato cha nne .
• Awe ana akili timamu na uwezo wa kujieleza inapobidi.
• Awe anajua kuongea vizuri lugha ya Kiswahili .
• Awe na umri sio chini ya miaka 18.
• Awe anatumia dawa za VVU.
• Awe amefanya kazi ya kuhudumia watu wanaoishi na magonjwa sugu (VVU) kwa miaka zaidi ya mitatu.
• Awe ana uwezo wa kutoa elimu kuhusu VVU na umuhimu wa kuhudhuria clinic kama alivyopangwa .
• Awe na uwezo wa kuhamasisha /kushawishi umuhimu wa kujua afya kwa kupima VVU kifamilia.
• Awe na uwezo wa kutembelea wateja wanaohitaji msaada wake wakati wowote bila kutoa vipingamizi.

• Awe na uwezo wa kuwatia moyo wateja waliokata tamaa ya kuishi kwa kukataa kunywa daw za VVU.
• Awe na uwezo wa kushirikisha / kutoa taarifa kwa viongozi ili kupata ufumbuzi wa shauri.
• Kigezo cha mafunzo ya Huduma ngazi ya jamii kitapewa kipaumbele
• Awe na barua ya utambulisho kutoka kwa mtendaji wa eneo analoishi.

Maombi yatumwe kwenye anuani ifuatayo:
Mkurugenzi
Baylor College of Medicine Children’s
Foundation – Tanzania
S.L.P 2663, Mbeya Tanzania
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11/3/2020
Email hr baylortanzania.or.tz
Location Mbeya
Deadline 2020-Mar-11

The post Nafasi za Kazi Baylor College of Medicine Childrens Foundation, Tuma Maombi Kabla ya Tarehe 11 March 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Nafasi za Kazi Baylor College of Medicine Childrens Foundation, Tuma Maombi Kabla ya Tarehe 11 March 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/12665/