Saturday, January 18, 2020

Names Called for Interview(MU & TGFA) 24 January 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.NaEA.7/96/01/K/141 16 JANUARI, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU) na Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote wa Mamlaka hizi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 24 Januari, 2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-

i. Usaili wa Mahojiano utafanyika tarehe 24 Januari, 2020 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili.
ii. Muda na sehemu ya usaili ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji pamoja na “Academic Transcript”;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional
Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha
IV na VI (form iv and form vi results slips) HAVITAKUBALIWA
NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na
NECTA); na
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji yaTangazo husika.
xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za
Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili
pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

KUSOMA MAJINA HAYO PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Names Called for Interview(MU & TGFA) 24 January 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Names Called for Interview(MU & TGFA) 24 January 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/8960/