Thursday, September 3, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Tanesco Tarehe 09 hadi 29 Septemba,2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAISSEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/2760

2 Septemba, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya SHIRIKA LA UMEME TANZANIA(TANZANIA ELECTRICSUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 09 hadi 29 Septemba,2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi Waombaji Kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i.Usaili utafanyika kuanzia tarehe 09 hadi 29Septemba, 2020 kamailivyo oneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwakila Kada;
ii.Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa Mchujo na kwa Madereva wenye usaili wa Vitendo pia, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya kazi
iii.Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask);
iv.Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwaajili ya utambuzi;
v.Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
-Kitambulisho cha Mkazi,
-Kitambulisho cha Mpigakura,
-Kitambulisho cha kazi,
-Kitambulisho cha Uraia au
-Hatiyakusafiria;
vi.Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vii.Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
viii.Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi
ix.Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipo pangiwa kufanyia usaili;
x.Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlakahusika(kama TCU, NACTE auNECTA);
xi.Waombajikazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawa kukidhivigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazohusika
xii.Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi
xiii.Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao katika mfumo wa maombi ya kazi na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili

KUSOM A MAJINA NA TAREHE PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Tanesco Tarehe 09 hadi 29 Septemba,2020 appeared first on Business Solutions.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Tanesco Tarehe 09 hadi 29 Septemba,2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/22424/