Monday, August 3, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili huo Cha Uhasibu–Arusha (IAA) Tarehe 10 hadi 11 Agosti, 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/2571

Agosti, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo Cha Uhasibu–Arusha (The Institute Of Accountancy Arusha)(IAA) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 10 hadi 11 Agosti, 2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofahulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezoyafuatayo:
i.Usaili utafanyika kuanzia tarehe 10 hadi 11Agosti, 2020 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili;; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kilaKada;;
ii.Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa mchujo na kwa Madereva wenye usaili wa Vitendo pia, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombiya kazisehemu ya ‘My Application.’
iii.Kilamsailiwaanatakiwakufikakwenyeeneo la usailiakiwaamevaaBarakoa (Mask);;
iv.Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwaajiliya utambuzi;;
v.Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:-¬Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hatiyakusafiria;;
vi.Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemea na na sifa za Mwombaji;;
vii.Wasailiwa watakao wasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;;
viii.Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;;
ix.KilaMsailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;;
x.Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikisheVyetivyaovimehakikiwanakuidhinishwanaMamlakahusika(kama TCU, NACTE au NECTA);;
xi.Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapo tangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazohusika.
xii.Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyiakazi.
xiii.Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili

KUSOMA MAJINA NA RATIBA PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili huo Cha Uhasibu–Arusha (IAA) Tarehe 10 hadi 11 Agosti, 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili huo Cha Uhasibu–Arusha (IAA) Tarehe 10 hadi 11 Agosti, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/20398/