Friday, June 12, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tarehe 20 na 23 Juni, 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA MOROGORO

Kumb. Na: S.10/MMC-28/VOL.IV/87

Tarehe: 12 Juni, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro anapenda kuwatangazia waombaji wote walioomba kazi ya Mtendaji wa Mtaa Daraja III kuwa Usaili utafanyika tarehe 20 na 23 Juni, 2020 saa 1:00 asubuhi katika Chuo Kikuu Jordan (HEKIMA HALL).

Aidha Usaili wa Mchujo (Written Interview) utafanyika tarehe 20/06/2020 na wasailiwa watakaofaulu ndio watakaochaguliwa kuendelea na Usaili wa Mahojiano (Oral Interview) tarehe 23/06/2020 katika Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro siku ya Jumanne kuanzia saa 1:00 Asubuhi.

Orodha ya waombaji walioitwa kwenye usaili ni kama inavyoonekana hapo chini, kwa waombaji ambao majina yao hayakuonekana katika orodha hiyo watambue kuwa maombi yao hayajakidhi sifa kwa mujibu wa nafasi zilizotangazwa. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro anawashukuru kwa kuleta maombi ya kazi na wasisite kutuma maombi tena kipindi Halmashauri itakapotangaza nafasi za kazi ambazo zitaendana na sifa walionazo. Waombaji wote walioitwa kwenye usaili wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Wasailiwa wafike na Vyeti Halisi (Original) vya Taaluma, Kuzaliwa, Vyeti vya Shule na Kitambulisho.
ii. Vitambulisho vitakavyokubaliwa ni pamoja na Kitambulisho cha Uraia, kitambulisho cha Kupiga Kura, Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria.
iii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA).
iv. Msailiwa anayekuja kufanya usaili atajigharamia mwenyewe
v. Msailiwa anatakiwa kuzingatia tarehe, muda na eneo la usaili
vi. Usaili utafanyika kwa njia ya maandishi na mahojiano
vii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask) na kuzingatia maelekezo yote ya kujikinga na Corona.
viii. Tahadhari usaili utafanyika kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma, kuna matapeli wanaotumia majina ya watu na vyeo vya watu kwa lengo la kujipatia fedha kuweni makini na matapeli hao.

OFISI HAITAWASILIANA NA MSAILIWA YEYOTE KWA NJIA YA SIMU.

KUSOMA ZAJINA HAYO PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tarehe 20 na 23 Juni, 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tarehe 20 na 23 Juni, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/18147/