Wednesday, June 3, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) Tarehe 09 hadi 10 Juni, 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/210

3 Juni,2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 09 hadi 10 Juni, 2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 09 hadi 10 Juni, 2020 kama ilivyo oneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
ii. ii. Kila Msailiwa anapaswa kunakili namba ya kufanyia Usaili aliyotumiwa kwenye akaunti yake ya maombi ya kazi na kuja nayo wakati wa Usaili wa Mchujo.
iii. iii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask);
iv. iv. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
v. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:-Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
vi. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vii. vii. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
viii. viii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
ix. ix. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
x. x. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA);
xi. xi. Waombaji kazi ambao majinayao haya kuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

PAKUA PDF HAPO CHINI KUSOMA RATIBA NA MAJINA

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) Tarehe 09 hadi 10 Juni, 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) Tarehe 09 hadi 10 Juni, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/17679/