Saturday, May 16, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili huo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Tarehe 20 – 21 Mei 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) anapenda kuwataarifu Waombaji kazi waliotuma maombi
ya kujaza nafasi wazi za kazi za Wanataaluma kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa tarehe 20 Mei, 2020 na 21 Mei, 2020. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika tarehe 20 Mei, 2020 kwa mchujo na Mahojiano 21 Mei, 2020 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili;
ii. Kila Msailiwa anatakiwa kufika eneo la usaili akiwa amevaa barakoa na kuzingatia maelekezo yote ya kujikinga na corona;
iii. Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Idara;
iv. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
v. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
vi. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti
cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu,
Shahada nakuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vii. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form
iv and form vi results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
viii. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
ix. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
x. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA); na
xi. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya Tangazo
husika.
xii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
xiii. Kutokana na kujikinga na ugonjwa hatari wa Corona unaoambukizwa na virusi vya COVID 19 Kila Mtahiniwa anatakiwa kuja kwenye usaili akiwa amevaa barakoa

KUSOMA MAJINA PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili huo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Tarehe 20 – 21 Mei 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili huo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Tarehe 20 – 21 Mei 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/16944/