Friday, April 3, 2020

Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III (Nafasi 7) Wilaya ya Hanang, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 16 April 2020

OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA HANANG

Unapojibu Tafadhali taja
KUMB N HAN/DC/E.2/1/VOL II/6

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Hnang impeta kibali cha ajira mbadala chenye kumbukumbu namba FA.170/448/01/2125 Cha tarehe 5 Machi 2020 kwaajili ya kuajiri watumishi 7 kujaza nafasi ya kazi Mtendaji wa Kijiji III

Hivyo Mkurugenzi anatangaza nafasi hizo kwa watanzania wenye sifa zilizoorodheshwa katika tangazo hilo ili wawasilishe maombi yao

AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III NAFASI 7

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Mwombaji awe na elimu ya kidao cha 4 au sita alyehitima mafunzo ya astashahada/cheti katika moja ya fani zifiatazo
  • Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi w fedha, maemdeleo ya jamii na sayansi ya sanaa katika chuo cha serikali za mitaa Hombolo Dodoma au chuo knachotambulika n na serikali

MAJUKUMU

  1. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
  2. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa amani na
    Msimamizi wa utawala bora katika Kijiji;
  3. Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji;
  4. Katibu wa Mikutano ya Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
  5. Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  6. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi
    katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza
    uzalishaji mali;
  7. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalam katika Kijiji;
  8. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji; na
  9. Kutekeleza shughuli nyingine atakazopangiwa na Mwajiri.

MSHAHARA
Kwakuzingatia ngazi ya mshara wa Serikali yaan TGS B

MAELEKEZO YA JUMLA

  • waombaji wawe raia wa Tanznia na wenye umri wa kuanzia miaka 18 – 45
  • maombi yaambatanishwe na taarifa ya maelezo binafsi (CV) YA Muombaji ikionyesha wadhamini watatu na taarfia zao sahihi namba za simu za muombaji na wadhamini cheti cha taaluma cheti cha kidato cha 4 cheti cha kuzaliwa picha 2 passpoert size za hivi karibuni ziandikwe majina kwa nyuma
  • testmonial na provisional statement of results , hati ya matokeo ya kidato cha 4 na 6 havitakubaliwa
  • waombaji waliostaafu/staafishwa au kuacha kazi katika utumishi wa umma hawataruhusiwa kuomba isipokuwa kwa kibali cha katibu mkuu kiongozi
  • muombaji atakaye wasilisha taarifa na sifa za kughushi atachukuliwa hatua za kishera kwa mujibu wa utaratibu
  • barua ziandikwe kwa mkono na kwa lugha ya kiswahli au Kingereza
  • waombaji waliopo katika utumishi wa umma wapitishe barua zao kwa waajiri wao
  • muombaji awe hajawahi kupatikana na kosa lolote jinai au kufnugwa jela
  • waombaji waliosoma nje ya nch iwaambatanishe vytei vyao ulinganifu kutoka baraza la mitihani tanzania
  • mwisho wa ktuma maombi ni Tarehe 16/04/2020
  • maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo

MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA,
HALMASHAURI YA WILAYA YA HANANG,
S.L.P 2
KATESH- HANANG

The post Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III (Nafasi 7) Wilaya ya Hanang, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 16 April 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III (Nafasi 7) Wilaya ya Hanang, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 16 April 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/15043/