Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) Tarehe 11 hadi 24 Machi, 2020
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.Na.EA.7/96/01/K/9170 02 MACHI, 2020
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi waliotuma maombi ya kujaza nafasi wazi za Mamlaka hiyo kuwa, usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 11 hadi 24 Machi, 2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 24 Machi, 2020 kwa mujibu wa ratiba kwa kila kada kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili.
ii. Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila kada;
iii. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Ashashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada nakuendelea kutegemeana na mahitaji ya tangazo la kazi na sifa za Mwombaji;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form IV and
form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA
KUENDELEA NA USAILI;
vii. Waombaji kazi wa nafasi ya “Conservation Ranger III – Wildlife Management- Law Enforcement” wanatakiwa kuripoti kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro – Arusha tarehe 10 Machi, 2020 na watakapokuwa kambini watagharamiwa malazi na chakula kwa siku zote.
viii. Waombaji kazi wa “Conservation Ranger III- Boat Operator” wanatakiwa kuripoti Ofisi za TANAPA mkoa wa Mwanza kwa tarehe iliyopangwa kwa usaili wa vitendo;
ix. Waombaji kazi wa kada ya “Conservation Ranger III- “Plant Operator” wanatakiwa kuripoti ofisi za TANAPA Makao Makuu – Arusha kwa tarehe
iliyopangwa kabla ya kuelekea kwenye usaili wa Vitendo kwa ajili ya maelekezo zaidi;
x. Waombaji kazi wa kada nyingine zote watajigharamia kwa usafiri, chakula, na
malazi;
xi. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanya usaili;
xii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA);
xiii. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi
za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika; na
xiv. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma
wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za
kufanyia kazi.
KUSOMA MAJINA HAYO BOFYA PDF HAPO CHINI
The post Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) Tarehe 11 hadi 24 Machi, 2020 appeared first on Ajira Zetu.
The post Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) Tarehe 11 hadi 24 Machi, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.
source http://ajira-nafasizakazitz.com/12755/