Thursday, February 27, 2020

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Tarehe 6 hadi 10 Machi, 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/167 26 Februari, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Chuo cha Bahari (DMI),
Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (CARMATEC), Kituo cha Matibabu cha Kikristo Kilimanjaro (KCMC), Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 6 hadi 10 Machi, 2020 na hatimaye kuwapangia
vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 6, Machi, 2020, usaili wa vitendo utafanyika tarehe 6, 7 na 9 na usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 9 hadi 10 Machi, 2020 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na mahitaji ya tangazo la kazi na sifa za Mwombaji;
v. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of
results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form iv and form vi results slips)
HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
viii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA);
ix. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika; na
x. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa
kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

DOWNLOAD PDF FILE HERE.

The post Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Tarehe 6 hadi 10 Machi, 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Tarehe 6 hadi 10 Machi, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.



source http://ajira-nafasizakazitz.com/12441/